Kurasa

Jumapili, 21 Juni 2015

Kenya thrash Algeria to qualify for FIVB World Cup


Kenya national volleyball team celebrates after
Kenya national volleyball team celebrates after winning the Women's Africa Nations Volleyball championship against Algeria at Safaricom Indoor Arena in Nairobi on 20th June 2015 . PHOTO | MARTIN MUKANGU | NATION 


Kenya safely navigated through a couple of challenges from Algeria to claim a record ninth continental women volleyball crown, following an exciting contest at the Safaricom Indoor Arena in Nairobi on Saturday.

SLAA,PRO JAY,CHRISTIAN BELLA,SUGU,MDEE KUISIMAMISHA DAR LEO




KATIKA kuendeleza harakati za kumkomboa mwanamke kwenye vishawishi na rushwa mbalimbali kutoka kwa viongozi wa kisiasa, Balaza la Wanawake Chadema (BAWACHA) limegundua mbinu mpya.

Mbinu hiyo inalenga kushawishi wanawake kuchukia na kukataa rushwa ili kuweza kuchagua viongozi wenye maadili. Harakati hizo zitafanywa kati ya BAWACHA na Wanawake Bendi. 

Imefahamika kuwa, wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wanawake wanaoonekana kuwa na ushawishi kubwa, hutumia kuwapotosha wanawake wenzao na hata kupokea rushwa kutoka kwa viongozi.

Lakini pia wanawake huchukuliwa kama watu wa mwisho ambapo hufanyiwa maamuzi na wanaume hasa kipindi cha uchaguzi.

Jumatano, 17 Juni 2015

Wema Sepetu kathibitisha anagombea Ubunge !!


Wema Sepetu kathibitisha anagombea Ubunge !! kayazungumza hapa na ya boyfriend wa Linah.
staa wa movies nchini Tanzania Wema Sepetu
Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Abraham Sepetu leo June 16 kupitia kipindi cha Ala za Roho ya Clouds FM amefunguka kuhusiana na kuchukua fomu ya ubunge wa viti maalumu mkoani Singida pamoja na ishu ya kutoka na boyfriend wa msanii Linah.
Akizungumza na Diva Loveness wa Ala za Roho alisema..”Sasa hivi niko singida kwenye maandalizi ya kuchukua fomu kwasababu nagombea ubunge wa viti maalumu mkoa wa singida, kwa hiyo nimekuja huku kuja katika kuamasisha vijana wajitokeze kujiandikisha kwenye daktari la kupigia kura, nimekuja kujiandikisha huku kwa sababu mama yangu ni mtu wa singida so nimejiandikisha tayari tukutane 15 tena kuja kuchukua fomu, kwasababu fomu zinatoka tena tarehe 14 mwezi wa saba so inshallah tuombe uzima, kampeni zimeshaanza zile ndogo ndogo nashukuru Mungu naendelea vizuri nahitaji support kwa jamii
Diva:“…I Know about kampeni za chini chini ambazo ulikuwa unafanya kwa muda mrefu kwaajili ya kugombea Ubunge na umepiga picha kwa Raqay tayari ukiwa na mavazi ya CCM si ndio kampeni pale iko pale pale au??…”
Wema:“…. Yes nimefanya so ama nilikuwa nazungumza na mangement yangu ambayo yupo Martin kadinda na pia yuko Petiman  ambaye yupo katika suala zima la kampeni yangu so watanzania wajue tu yes  nitachukua fomu ya kugombea Ubunge wa viti maalumu ya mkoani Singida and tutaona uko mbele itakavyokuwa kwasababu hiki ni kinyang’anyiro naingia katika ni kama vile naingia kwenye mapambano yaani vitaani so kuna kupata na  kukosa lakini si fikiri kukosa kwasababu mtu ukifikiri kukosa unajiweka kwenye negative side sana lakini najua kwa nguvu za watanzania na kwa nguvu za wananchi wa Singida wataweza kuniamini na kunipa kura zao.
Katika mahojiano hayo Diva alimuuliza Wema Sepetu kuhusu ishu ya kuwa na mahusiano na boyfriend wa Lina alisema”...Huwezi amini hizo habari si za kweli kwasababu tulikuwa tunafanya project  zinakuja ila nimeshangashwa kuona kwanini Lina ameenda on air kwenye kipindi na kuzungumz

Jumanne, 9 Juni 2015

Rachel Njingo kutoka October 3 mwezi huu!

Sexy lady mtafutaji anayejishughulisha na fani lukuki ikiwemo urembo, filamu na muziki, Rachel Njingo  kwa mara njingine mwishoni mwa mwezi huu anakuja na filamu October 3.Filamu ukiwa imetayarisha na Jay Bonge wa J Bongo movies imeshirikisha wasanii wa wakali wa filamu Afrika Mashariki na kati wakiwepo Jengua, Rachel Njingo na wasanii wengine wengi. 
 
Rachel Njingo katika pose
Akigungumza na blog  http://batarokota.blogspot.com/ Rachel Njingo alisema `filamu mpya inakuja nimeshirikishwa na Jay Bongo na inaitwa  October 3 filamu hii inatarajia kuwa hewani mwezi huu Mwisho, hivyo washabiki wangu wasubirie ujuo wa filamu hii kwa hamu` alisema Rachel Njingi akiwa Dodoma nchini Tanzania.

Jumapili, 7 Juni 2015

ZA MWIZI 40! DENTI CHUO KIKUU ANASWA


Kibano! Njemba mmoja almaarufu kwa jina la Babuu amenaswa kisha kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kuvunja na kuiba kompyuta mpakato (laptop) nyumbani kwa mtu, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda kamili.
 
Mwizi maarufu alifahamika kwa jina la babuu pichani akiwa amewekwa chini ya ulinzi na raia wenye hasira kali.
Tukio hilo la kinyama lililoshuhudiwa na Makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers lilijiri wikiendi iliyopita, majira ya saa 8:00 mchana kweupe, maeneo ya Mwenge jijini Dar ambapo OFM, wakiwa ‘wanarandaranda’ kusaka matukio, walisikia sauti za ‘mwiziii...mwiziii...mwiziii..’ na kushuhudia umati ukimuangushia kipigo mtu huyo waliyedai aliiba laptop hiyo kwenye nyumba moja iliyopo eneo hilo.
 
Babuu pichani akitoa maelezo baada ya kupewa kichapo na raia kwa madai ya kuiba laptop aina ya Apple.
Katika utetezi wake, jamaa huyo alidai yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja maarufu jijini Dar (jina tunalo) na kudai kuwa laptop hiyo aliichukua kwa mtu ambaye anamdai aliyemtaja kwa jina moja la Ford.
Wananchi hao waliokuwa wakimsulubu walikuwa wakipingana wengine wakidai kuwa madai ya mtu huyo yanapaswa yachunguzwe kwanza kabla ya kupigwa, huku wengine wakitaka auawe kwani alikiri kuchukua laptop isiyo yake.
 
Mwizi huyo akiwa nje ya chumba alichofanyia uhalifu na kuonyesha baadhi ya vifaa alivyoiba.
 
Raia wakimhoji babuu baada ya kumkamata na laptop.
 
Mwizi huyo akiendelea kupokea kichapo.
Hata hivyo, watu hao walikubaliana kumpeleka mtuhumiwa huyo hadi kwenye nyumba anayodaiwa kuvunja na kwenda naye ‘msobemsobe’ ambapo watu walishuhudia mlango wa chumba cha mtu ambaye hakuwepo muda huo, ukiwa wazi na kitasa kikiwa chini ukiashiria kuvunjwa.
Kama hiyo haitoshi, Babuu, katika harakati za kukurupuka eneo hilo aliacha begi lenye laptop tatu ambapo moja alikiri kuichukua kutoka ndani ya chumba hicho.
Mbali na laptop hizo, njemba huyo alikutwa na bisibisi na funguo zaidi ya 18 za vitasa tofauti huku funguo moja ikitajwa kama ‘funguo malaya’ ambayo hufungua kitasa chochote.
Baada ya kumnasa na funguo hizo, wananchi hao walimvua nguo na kumuacha akiwa na ya ndani pekee huku baadhi yao wakiomba wamfanyie ‘kitu mbaya’ lakini machozi yake na kuloa damu chapachapa vikamuokoa.
Kama upepo taarifa zilifika kwa mwenye chumba ambaye alifika na kudai kuwa hamfahamu mtu huyo ndipo kipigo cha kufa mtu kikaendelea huku umati ukiruka ukuta wakitaka kutoa adhabu kila mmoja kwa mtindo wake.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Chacha alifika eneo la tukio na kukiri kupata malalamiko ya mara kwa mara ya wizi wa majumbani kutoka kwenye nyumba hiyo ambapo wizi huwa ni wa mashuka na nguo ambazo huanuliwa zikiwa zimeanikwa.
Mwenyekiti huyo alitumia busara kuwazuia watu wasimpige jamaa huyo kisha kuwataarifu polisi waliofika eneo la tukio na kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi na matibabu.

Jumamosi, 6 Juni 2015

NISHA AWASHTAKIA WEZI KWA MUNGU



Baada ya wezi kumfanyia kitu mbaya kwa kumuibia vifaa kibao kwenye gari lake na kuliacha kama gofu, staa wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameamua kufunga siku saba kwa ajili ya kuwashtaki wezi hao kwa Mwenyezi Mungu.
 
Staa wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Akizungumza na paparazzi wetu, Nisha alisema kwa siku hizo saba ataomba dua maalum na hatatoka nyumbani kwenda sehemu yoyote na hii ni kwa ajili ya kuwashtakia kwa Mungu wale waliomuibia vifaa vya gari na fedha kwani anajua dua ndiyo kila kitu.
“Niko kwenye mfungo wa siku saba kwa ajili ya kuwashtaki wale walioniibia maana najua Mungu ndiye aliyenipa na hao walioniibia atawalipa sawasawa na ubaya wao, sijafanikiwa kumjua hata mmoja lakini najua Mungu anawajua na atawalipa kwa wakati wake,” alisema Nisha.

Rachel Njingo Mrembo mwenye vipaji rukuki


Ukiachilia mbali kucheza filamu mbalimbali Rachel Njingo anafanya vizuri pia katika modelling. Utaweza kumuona katika video ya wimbo wa PNC  - Yule Yule amecheza kama video Queen wa wimbo huo. Lakini kwa sasa amejikita zaidi katika filamu na ndoto yake kubwa ni kuja kufanya filamu moja na Jackline Wolper.
Rachel B. Njingo akiwa na Jackline Wolper.

Rachel Njingo: Naja na Kidudumtu Filamu

Muigizaji wa filamu Tanzania na Afrika Mashariki, Rachel Njingo, ameibuka filamu mpya Kidudumtu. Katika filamu ya Kidudumtu Rachel Njingo ameshirikiana na wasanii mbalimbali wakiwemo Jack Chaz, Haji Adamu, Halima Yahaya, Jack Chat, Piere Joseph Ahmrd Makambaza.

Rachel Njingo alidai baada ya kuakaa kwa muda mrefu na akitamba na filamu ya CLARITHA iliyoshika vilivyo soko la filamu Afika Mashariki na Kati na sasa aja na ujuo mpya ma  kutoka na filamu ya Kidudumtu filamu inayo tarajia kutoka hivi karibu nchini Tanzania.
Rachel, alisema "kimya chake cha muda baada ni kutoka na kuanda filamu mpya ya Kidudumtu ambayo inakaribia kutoka hivi karibuni .alisema  nashukuru Mungu nimemaliza filamu mpya ya Kidudumtu salama na naomba watu waisubirie ujio mpya," aliongeza Rachel Njingo.