Kurasa

Jumatano, 3 Juni 2015

Rachel Njingo: Filamu zimeponitezea ndoto ya uwanasheria.



Muigizaji wa filamu Tanzania, Rachel Njingo, amesema kuwa kujiingiza katika filamu ndiko kulikozima ndoto zake za utotoni za kuwa mwanasheria.
Rachel alidai kuwa wakati akisoma udogoni lengo lake kubwa lilikuwa ni kuja kuwa mwanasheria kwani ndio kazi aliyokuwa akiipenda na aliamini kwamba ndoto yake ingetimia siku moja.
Lakini mwanadada huyo alisema kila kitu kiliharibika baada ya kujiingiza katika filamu na kujikuta sasa maisha yake yapo kwenye filamu zaidi.
Rachel, alisema  "Lakini baada ya kuanza kuigiza nikaona watu wananikubali na kupenda kile nikifanyacho, ndipo nilipoanza kupata mafanikio nikaona OK, kumbe hii ni kazi, nikaanza kuifanya kwa umakini zaidi," 
Rachel alisema "kimya chake cha muda baada ni kutoka na kuanda filamu mpya ya Kidudumtu ambayo inakaribia kutoka hivi karibuni .alisema  nashukuru Mungu nimemaliza filamu mpya ya Kidudumtu salama na naomba watu waisubirie ujio mpya," aliongeza Rachel Njingo.