Q-Chillah akielezea namna alivyojipanga kwa ujio wake mpya. Kushoto ni Meneja wake, QS. Mhonda.
Wasanii Luten Karama kushoto, Isabella Mpanda katikati pamoja na Baby Madaha wakiwa katika picha ya pamoja.
Wasanii wakiwa katika pozi, wapili kutoka kulia ni Q-Chillah akifuatiwa na Dully Sykes.
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ amesema hategemei kupotea tena kutokana na ujio wake mpya katika gemu baada ya kupotea kwa muda mrefu.
Q-Chillah ameyasema hayo jana usiku katika Hoteli ya Star City jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua video zake mbili zinazokwenda kwa jina la For U pamoja na Power of Love.
Alisema kwa sasa amefanikiwa kumpata meneja wake mwenye kutambua vipaji vya wasanii hasa katika kuviendeleza akimtaja kwa jina la Joseph Mhonda ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya QS. Mhonda.